HABARI TATU BOMBA KUTOKA KWENYE MAGAZETI YA LEO. - LEKULE

Breaking

17 Jan 2016

HABARI TATU BOMBA KUTOKA KWENYE MAGAZETI YA LEO.

1. Ukawa waikamata Dar es Salaam..
Kwa vyovyote vile hii ni habari kubwa inayopewa nafasi ya kwanza na mtandao wa mjengwablog.com. Tumepata kuchambua, kuwa umeya Dar unapaswa kuangaliwa katika picha kubwa. Ifahamike, Dar ni 'mkoa wa kitaifa' na kuwa meya Dar ni nafasi kubwa sana kitaifa. Si ajabu, kuwa vita haikuwa ndogo, baina ya upinzani na chama tawala, katika Hii ni vita ya kuipigania Dar.
CCM kupoteza nafasi za umeya kwa Ilala na Kinondoni kwaweza kutatafsiriwa kama kupoteza nguvu zake za kisiasa ndani ya jiji kitovu cha siasa na biashara hapa nchini. Ingawa, matokeo hayo yanaweza pia kuipa nafasi CCM kuonyesha uwezo wake wa kuendesha siasa za upinzani dhidi ya halmashauri zenye kuongozwa na vyama pinzani. Kuonyesha mbadala wakiwa nje.
Naam, demokrasia imechukua mkondo wake, ni wakati sasa wa waliochaguliwa kuendesha halmshauri kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi kwa kushirikiana na Serikali Kuu iliyo madarakani.
Na katika kuimarisha ubora wa uwakilishi wa watu, kama tulivyopendekeza juma moja lililopita, kuwa huko tuendapo ungekuwepo utaratibu wa meya kuchaguliwa na wakazi wenyewe kwa kupigiwa kura, na si kundi dogo la madiwani.Ndivyo wafanyavyo wenzetu walioendelea.
2. TCRA kuvifungua vituo 6 vya TV na redio 20
Hii ni habari inayochukua nafasi ya pili kwa mujibu wa mtandao waMjengwablog.com. TV na redio ni vyombo vyenye kuhusu jamii pana katika kupata habari na hata burudani. Inaripotiwa kuwa wahusika hawajalipa ada wanazopaswa kulipa. Imeandikwa pia, kuwa ifikapo kesho saa sita, kama hawajalipa, vituo vyao vitafungwa. Na baadhi ya wahusika wameonyesha kutofautiana na TCRA, ni kupitia kwenye magazeti, si redio wala tv, iwe za kwao au za washindani wao wengine kibiashara!
3. Polisi yawasaka wahariri Mawio

Ni habari itakayowavuta wasomaji wengi. Nasi mtandao wamjengwablog.com tunaipa nafasi ya tatu kwa ukubwa.

No comments: