Donald Tusk aishinikiza EU kudhibiti mgogoro wa uhamiaji - LEKULE

Breaking

20 Jan 2016

Donald Tusk aishinikiza EU kudhibiti mgogoro wa uhamiaji

Wahamiaji waliozuiliwa na vikosi vya usalama vya Hungary baada ya kuvuka  uzio wa nyaya za chuma uliojengwa kwenye mpaka kati ya Serbia na Hungary, Jumanne 15 Septemba 2015.
Wahamiaji waliozuiliwa na vikosi vya usalama vya Hungary baada ya kuvuka uzio wa nyaya za chuma uliojengwa kwenye mpaka kati ya Serbia na Hungary, Jumanne 15 Septemba 2015.

Na RFI
Umoja wa Ulaya hauna "zaidi ya miezi miwili" ili kudhibiti mgogoro wa uhamiaji au utapata athari katika eneo la Schengen kwa uhuru wa kutembea kwa watu na mzunguko wa vitu, amesema Jumanne hii rais wa Baraza la Ulaya, Donald Tusk mbele ya Bunge la Ulaya.
"Baraza la mwezi Machi liitakuwa fursa ya mwisho ili kuona kama mkakati wetu unafanya kazi. La sivyo, tutakabiliana na matokeo mabaya kama vile kuanguka kwa Schengen", Donald Tusk amesema.
Donald Tusk pia ameonya dhidi ya hatari ya kushindwa kwa "mradi wa kisiasa" wa Umoja wa Ulaya kama jamii nzima itashindwa kudhibiti ukaguzi wa mipaka yake ya nje.
Ulaya inakabiliwa tangu mwaka jana na mgogoro mbaya wa uhamiaji. Mgogoro kama huo ulitokea mwishoni mwa Vita vikuu vya pili.
Rais wa Tume ya Ulaya, Jean-Claude Juncker, ametoa kauli pia ya tahadhari, akizitolea wito nchi wanachama kutekeleza mikakati iliyopendekezwa na mkutano wao wa pamoja: kuundwa kwa kikosi cha walinzi wa mipaka ya Ulaya, vituo vya ukaguzi au "hot spots" katika mipaka ya nje na kutambua maeneo wanakoishi wakimbizi katika nchi wanachama.
Hungary, Slovenia, Austria, Denmark na Sweden tayari wameanzisha utaratibu wa ukaguzi kwenye mipaka.
"Mipaka ya pamoja, usimamizi wa pamoja. Kama hatutatekeleza hilo, Schengen haina muda mrefu wa kuishi", Donald Tusk amesema.

"Tume ya Ulaya tayari iliwasilishwa mambo yote yanayohitajika ili kusimamia mgogoro wa wakimbizi", Tusk amebaini, huku akitoa wito kwa nchi wanachama kutekeleza mambo hayo tangu sasa na kupata "mafanikio ya ujenzi wa Ulaya"

No comments: