DKT. TIBOROHA AJIUZULU NAFASI YA UKATIBU MKUU WA YANGA - LEKULE

Breaking

24 Jan 2016

DKT. TIBOROHA AJIUZULU NAFASI YA UKATIBU MKUU WA YANGA

Dr. Jonas Tiboroha
Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga Dr. Jonas Tiboroha ametangaza kujiuzulu wadhifa wake ndani ya klabu hiyo ya Jangwani kutokana na fukuto kubwa lililopo kwenye uongozi wa juu wa klabu hiyo.
Mtandao huu umenukuu maelezo yaliyoandikwa kwenye page ya facebook ya ‘Naipenda Yanga’ ambayo kwa mujibu wa page hiyo, Dr. Tiboroha ametoa sababu kadhaa za kujiuzulu wadhifa wake ndani ya Yanga.
“Mimi ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitivo cha Elimu ya Viungo (PE), na kwa kuondoka Yanga SC maana yake napata wasaa mzuri wa kumtumikia mwajiri wangu, UDSM,” amesema.
Pamoja na Tiboroha kutozama ndani sana juu ya kujiuzulu kwake, lakini inaelezwa alikuwa hana maelewano na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya klabu ya Yanga, Isaac Chanji ambaye kwa sasa ndiye mtu anayesikilizwa na kuaminiwa zaidi na Manji.
Tayari Jonas Tiboroha amewasilisha barua ya kujiuzulu kwa Mwenyekiti Yusuf Manji.

No comments: