Chenge Awapa Somo Wabunge Kuhusu Matumizi ya Kanuni Za Bunge....Ni Baada ya Saed Kubenea Kuomba Mwongozo kuhusu Wabunge wa Kike Kuvuliwa Nguo - LEKULE

Breaking

30 Jan 2016

Chenge Awapa Somo Wabunge Kuhusu Matumizi ya Kanuni Za Bunge....Ni Baada ya Saed Kubenea Kuomba Mwongozo kuhusu Wabunge wa Kike Kuvuliwa Nguo

Mwenyekiti wa kikao cha Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge maarufu kwa jina la Mtemi amewataka wabunge kujifunza kwa umakini namna bora ya kutumia kanuni za Bunge.

Mwenyekiti Chenge amefanya hivyo mara kadhaa alipokuwa akijibu miongozo ya wabunge kutoka vyama vya upinzani wakiwamo Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea (CHADEMA), Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe (ACT) pamoja na Mbunge wa Singida Magharibi Tundu Lissu (CHADEMA).

Kwa upande wa kubenea aliomba muongozo kuhusu mbwa walioingizwa Bungeni, askari polisi kuwavua nguo za ndani wabunge wa kike pamoja na shanga na Hereni zao   jambo ambalo haliruhusiwi ambapo Mwenyekiti wa Bunge alimtaka mbunge huyo kutafuta kanuni nyingine ya kupeleka ombi lake kama anadhani hoja yake ni ya msingi.

Kwa upande wa Lissu pamoja na Zitto wenyewe waliomba miongozo kuhusu mpango wa serikali wa miaka mitano uliowasilishwa na serikali kupitia wizara ya fedha,kwamba umekiuka kanuni za bunge,ambapo mwenyekiti aliwajibu kwamba mpango haujakiuka na si mara ya kwanza kufanya hivyo na akaahidi kutoa  majibu baadae.

Aidha Mwenyekiti  huyo wa Bunge alitoa rai kwa wabunge wote kuzisoma kanuni za bunge na kuzielewa na mipaka yake katika namna bora ya kuendesha vikao hivyo vya Bunge.


Hata hivyo Kikao cha bunge kimeendelea kama kawaida na shughuli zake huku wabunge wa kambi rasmi ya upinzani wakirejea baada ya kugoma kushiriki katika mjadala wa kuijadili hotuba ya Rais kwa kigezo cha shirika la utangazaji la Taifa kutorusha matangazo ya moja kwa moja kuhusiana na mijadala hiyo

No comments: