CAR: Uchaguzi wa wabunge wafutwa - LEKULE

Breaking

26 Jan 2016

CAR: Uchaguzi wa wabunge wafutwa


Afisa wa Tume ya Uchaguzi akihesabu kura baada ya kufungwa kwa kituo cha kupigia kura katika mji wa Bangui, Desemba 30, 2015.
Afisa wa Tume ya Uchaguzi akihesabu kura baada ya kufungwa kwa kituo cha kupigia kura katika mji wa Bangui, Desemba 30, 2015.

Na RFI
Duru ya kwanza ya uchaguzi wa wabunge nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati umefutwa Jumatatu hii na Mahakama ya Katiba kutokana na"kasoro mbalimbali".
Mahakama ya Katiba imethibitisha pambano katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais kati ya Mawaziri Wakuu wawili wa zamani, Anicet Georges Dologuélé na Faustin Archange Touadéra.
Chaguzi hizi mbili, ambazo zinapelekea nchi hii maskini kuondokana na kipindi cha miaka mitatu ya vita na makabiliano kati ya jamii, zilifanyika Desemba 30 katika hali ya utulivu wa ajabu. Chaguzi hizi zilishuhudia kiwango kikubwa cha ushiriki wa wapiga kura licha ya matatizo mbalimbali ya vifaa.
"Uchaguzi wa (wabunge) wa Desemba 30, 2015 umefutwa nautarejelewa (...) kwa sababu ya kasoro nyingi na ushiriki wa wagombea katika kasoro hizo", Mkuu wa Mahakama ya mpito ya Katiba, Zacharie Ndoumba, amesema wakati wa mkutano wa hadhara jijini Bangui.
"Baraza la kitaifa la Mpito la (Serikali, bunge) litaendelea na shughuli zake mpaka Bunge jipya litakapochaguliwa na kuanza kazi", Zacharie Ndoumba ameongeza, akinaini kwamba mahakama "imepokea malalamiko 414" kutoka kwa wagombea waliofanyiwa unyonge.
Uchaguzi wa wabunge ulifanyika katika majimbo 140 nchini lakini vifaa vya uchaguzi na kadi nyingi za kupigia kura, vilivyosafirishwa katika dakika za mwisho, havikufika katika maeneo ya mbali.

No comments: