Baada ya David Beckham kusikia kuwa Zidane ameteuliwa kuwa kocha wa Real Madrid, haya ndio aliyoandika - LEKULE

Breaking

5 Jan 2016

Baada ya David Beckham kusikia kuwa Zidane ameteuliwa kuwa kocha wa Real Madrid, haya ndio aliyoandika



Baada ya kuwepo na tetesi za muda mrefu kuhusu uongozi wa klabu ya Real Madrid kutoridhishwa na mwenendo wa timu yao January 4, umetangaza rasmi kumfuta kazi aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Rafael Benitez. Real Madrid walitangaza kumfuta kazi Benitez na Zidane kutajwa kurithi nafasi hiyo kwa muda hadi mwisho wa msimu.

Kufuatia kuteuliwa kwa Zidane kurithi mikoba hiyo, stori zilimfikia mchezaji mwenzake wa zamani David Beckham na kuonesha furaha yake kwa kupost picha yao ya zamani na ujembe wenye kuoneshwa kufurahishwa na nguli huyo wa kifaransa kuchukua mikoba hiyoo.

“Unaweza kumpata mtu bora zaidi yake? mtu ambaye alikuwa bora kiwanjani na watu wote tunampenda, anachukua nafasi ya kutumikia klabu ambayo mimi na watu wengine tunaipenda, mtu mwenye passion na siku zote huwa hakubali kushindwa kwa namna yoyote ile. Kiukweli ni mtu sahihi kwa hiyo kazi” >>> Beckham

1
David Beckham na Zinedine Zidane waliwahi kucheza pamoja kwa miaka mitatu katika timu ya Real Madrid, baada ya David Beckham kuhama Man United na kuhamia Real Madrid mwaka 2003. Hata hvyo Jose Mourinho anatajwa kuhusishwa na Madrid kutaka kurudi mwishoni mwa msimu.

No comments: