ASKOFU PENGO AMEPONGEZA HUDUMA ZA TAASISI YA MOYO. - LEKULE

Breaking

9 Jan 2016

ASKOFU PENGO AMEPONGEZA HUDUMA ZA TAASISI YA MOYO.

SKOFU Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo jududi za madaktari na huduma zinazotolewa katika Tasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili.

Amepongeza leo wakati akizungumza  na waandishi wa habari Askofu Pengo pia amesema yeye alikua anaogopa kutokana na taarifa zinazotolewa kwenye vyombo vya habari juu ya Oparesheni tata iliyowahi kufanyika katika hospitali ya Taifa ya Mhimbili.

Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alilazwa katika taasisi ya moyo tangu Januari Mosi.

Kwa upande wa  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali imeokoa kiasi cha hilingi bilioni nne ambazo zilikua zipotee kwaajili ya kupeleka wagonjwa wa moyo kwenda kutibiwa  nje ya nchi.
 Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akingia katika ukumbi wa mikutano katika kitengo cha Moyo cha Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete kilichopo katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Ummy Mwalimu akimkaribishaAskofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ili aweze kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.


Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kuwapongeza jopo la Madaktari waliomhudumia katika Hospitali ya Mhimbili.
 Kulia ni aliyekuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwashamu Askofu Titus Mdoe na Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea, Damian Dallu wakiwa katika mkutano wa Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na waandishi wa habari katika ukumbi wa Mkutano wa Kitengo cha Moyo cha Jakaya Mrisho Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili.
 Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Ummy Mwalimu na Kushoto ni Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea, Damian Dallu.
 Katika mkutano huo  Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo  alitoa zawadi za kadi za pongezi kwa baadhi ya madaktari mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Ummy Mwalimu akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Mrisho Kikwete iliyopo katika hospitali ya Taifa ya Mhimbili, Profesa Mohamed Janabi. 

Katibu Mkuu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee Mpoki Ulisobisya akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusiana na swali lililoulizwa na mwandhishi wa habari kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee haitoi ruhusa ya mtu yoyote kwenda kutibiwa nje ya nchi na ruhusa hiyo hutolewa na Madaktari wenyewe ambao walikua wanamtibia mgonjwa.

No comments: