IMG_1422
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kubadilisha matumizi ya zaidi ya shilingi 60.6 milioni zilizokuwa zigharamie sherehe ya maadhimisho ya mkoa huu kutimiza miaka 50 toka uanzishwe mwaka 1963, na sasa zitatumika kununulia vifaa tiba na vitendea kazi katika hospitali mpya ya rufaa ya mkoa.
IMG_1426
IMG_1439
Meneja wa shirika lisilo la kiserikali la SEMA mkoani hapa, Ivo Manyaku, ameupongeza mkoa wa Singida kwa uamuzi wake wa kutumia shilingi 60.6 milioni zilizokuwa zitumike kwenye sherehe za maadhimisho ya mkoa kutimiza miaka 50, na kuamua kununulia dawa na vitendea kazi.
IMG_1481
Mfanyabiashara mjini hapa, Benard Sangawe,ununuzi wa dawa mbambali na vitendea kazi katika hospitali mpya ya rufaa ya mkoa, itasaidia kupunguza uhada wa vitendea kazi na dawa katika hospitali hiyo.MKOA wa Singida umefuta matumizi ya zaidi ya shilingi 60.6 zilizokuwa zitumike kugharamia sherehe za maadhimisho ya mkoa wa Singida kutimiza miaka 50 toka uanzishwe mwaka 1963,na badala yake sasa zitatumiwa kununua vifaa tiba na vitendea kazi katika hospitali mpya ya rufaa.
Imedaiwa kwamba uamuzi huo ni kuunga mkono falsafa ya rais Dk.John Pombe Magufuli ya kuachana matumizi yanayonufaisha watu wachache kwa muda mfupi,na kuzielekeza fedha husika katika kugharamia maendeleo ya wananchi wengi.
Hayo yamesemwa jana na mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone,wakati akiwatakia heri wananchi mkoani hapa kupitia vyombo vya habari.
Alisema kuwa ofisi yake iliwaita wadau mbalimbali kuwaomba wachangie kwa hali na mali maadhimisho hayo ambayo yalitarajiwa kufanyika Oktoba 15 mwaka huu,kwa moyo mkujufu walichanga shilingi 60,611,500/=.
“Lakini kwa bahati mbaya maadhimisho hayakufanyika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya tuliyemtarajia kuwa mgeni rasmi rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wakati huo,Jakaya Mrisho Kikwete kuwa na majukumu mengi ya kitaifa na kimataifa,na kushindwa kufika kama tulivyotarajia”,alisema Dk.Kone.
Alisema baada ya ofisi yake kubaini kuwa sherehe ya maadhimisho hayo imepitwa na wakati,tuliwaita wadau wote waliochangia na baada ya kukaa nao,kwa kauli moja,walikubali fedha hizo zitumike kununulia vifaa tiba na vitendea kazi.
Dk.Kone ametanguliwa na wakuu wa mkoa 17 hadi sasa toka mkoa wa Singida uanzishwe 1963.Hao ni toka mkoa wa Singida, Dantes Ngua akiwa Mkuu wa mkoa wa kwanza, wengine  ni Peter Kisumo, Rajabu Semvua, Kapilima Kapilima, Kingunge Ngombale Mwiru na Moses Nnauye.
Wengine zaidi ni Charles Kilewo, Brig Silas Mayunga, Abdallah Nungu, Capt Peter Kafanabo, Prof John Machunda, Maj Gen Mwita Marwa, Gallus Abeid, Abubakar Mgumia, Col Anatoly Tarimo, Halima Kasungu na Dk Parseko Kone aliyetumikia kwa kipindi kirefu kuliko wote.