WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR YASAINI MIKATABA MIWILI YA UJENZI NA MAKANDARASI M/S.HUMPHREY CONTRUCTION LIMITED YA ARUSHA NA MINDSET TECHIES (T) YA DAR ES SALAAM. - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Thursday, 31 December 2015

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR YASAINI MIKATABA MIWILI YA UJENZI NA MAKANDARASI M/S.HUMPHREY CONTRUCTION LIMITED YA ARUSHA NA MINDSET TECHIES (T) YA DAR ES SALAAM.

 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Khadija Bakari Juma akitoa ufafanuzi kwa Wadau waliohudhuria hafla ya Utiaji Saini wa Mikataba miwili ya Ujenzi baina ya Wizara yake na Makandarasi kutoka M/S. Hamphrey Construction Limited ya Arusha na Mindset Teches (T) ya Dar es Salaam Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Wizara ya Elimu Zanzibar.
 Wadau mbalimbali waliohudhuria katika sherehe za kutiliana saini mikataba hiyo.
  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Khadija Bakar Juma na Mkandarasi wa Kampuni ya M/s.Humphrey Construction Limited ya Arusha wakitiliana saini Mkataba wa kupanua Taasisi ya Maendeleo ya Utalii iliopo Maruhubi.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Khadija Bakar Juma na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi M/s. Humphrey Construction Limited ya Arusha wakibadilishana Mikataba baada ya kutiliana saini.
 Mkandarasi wa Kampuni ya M/s. Mindset Techies (T) Limited ya Dar es Salaam Thabit Kombi akitia saini Mkataba wa Ujenzi wa Kupanua Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume katika ukumbi wa Wizara ya Elimu Zanzibar.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Khadija Bakar Juma na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi M/s. Mindset Techies (T) Limited ya Dar es Salaam Thabit Kombi wakibadilishana Mikataba baada ya kutiliana saini.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya habari Utamaduni Na Michezo Zanzibar Issa Mlingot Ali akizungumza na Wadau waliohudhuria katika Mkutano huo.
Post a Comment