Waziri Lukuvi Asitisha Zoezi la Bomoa Bomoa Dar - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Wednesday, 23 December 2015

Waziri Lukuvi Asitisha Zoezi la Bomoa Bomoa Dar

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini, Mhe. William Lukuvi amesitisha zoezi la bomoabomoa kwa muda wa siku14 katika maeneo ya mabondeni na yaliyovamiwa na kujengwa kinyume cha sheria ili kutoa nafasi kwa watu waliojenga katika maeneo hayo kuondoa wenyewe mali zao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi imebainisha kuwa zoezi la bomoa bomoa limesimamishwa kwa muda kuanzia tarehe 22/12/2015 hadi 05/01/2016.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa eneo la mto msimbazi ni eneo hatarishi na ujenzi katika eneo hilo ni kinyume na sheria ya mipango miji na 8 ya mwaka 2007 na sheria ya mazingita na.4 ya mwaka 2004.

Maeneo mengine ambayo serikali imepiga marufuku ni maeneo ya wazi, kingo za mito, fukwe za bahari, maeneo ya hifadhi za barabara na maeneo hatarishi.

Aidha, katika Jiji la Dar es Salaam maeneo ya wazi takribani 180 yamevamiwa ambayo ni kama ifuatavyo; Halmashauri ya wilaya ya Kinondoni maeneo 111, Halmashauri ya Ilala maeneo 50 na Halmashauri ya Temeke maeneo 19.


Post a Comment