VIONGOZI WAPYA WA TAHLISO WAAPISHWA RASMI,WAUNGANA NA KASI YA MAGUFULI - LEKULE

Breaking

30 Dec 2015

VIONGOZI WAPYA WA TAHLISO WAAPISHWA RASMI,WAUNGANA NA KASI YA MAGUFULI

Mwenyikiti mpya wa shirikisho la wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania TAHLISO Ndugu STANSLAUS PETER akila kiapo kulitumikia shirikisho hilo mbele ya mwanasheria HAMZA JABIRI leo Jijini Dar es salaam kuanza kazi rasmi ya kuwatumikia wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania 

Uongozi mpya wa shirikisho la elimu ya vyuo vikuu nchini Tanzania TAHLISO umesema kuwa upo tayari kumuunga mkono Rais wa Tanzania Dr John pombe magufuli kwa kasi aliyoanza nayo na kuhakikisha kuwa elimu ya Tanzania hasa elimu ya vyuo vikuu inakuwa ya ubora unaofaa na inaheshimika nchini Tanzania.
Makamu Mwenyekiti mpya wa TAHLISO Ndugu JUMA ALLY OMARI akila kiapo leo jijini Dar es salaam 
Akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam katika hafla fupi ya kuwasimika viongozi wa shirikisho hilo wapya mwenyekiti mpya wa TAHLISO Tanzania Bw STANSLAUS PETER amesema kuwa kwa miaka mingi elimu ya juu nchini Tanzania imekuwa haina ubora unaotakiwa ikiwa ni pamoja na mitaala mibovu,ukosefu wa mokopo kwa wanafunzi wengi jambo linalowakatisha tamaa wengi kusoma,ambapo amesema uongozi wake umeona kasi nzuri ya serikali ya awamu ya tano na wapo tayari kushirikiana na serikali kutatua changamoto za wanafunzi nchini.
Naibu katibu mkuu wa TAHLISO KHAMIS ELLY akiapa leo Jijini Dar es salaam 
Mwenyekiti huyo amesema kuwa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka huu umeonyesha kuwa serikali ya Magufuli inawajali wanafunzi kwani asilimia kubwa ya wanafunzi walipata mikopo na wengine wanaendelea kupata mikopo huku akiwataka wanafunzi kutulia kwani neema kwao inakuja kutokana na kasi ya uongozi huo mpya pamoja na ule wa serikali ya awamu ya tano.
Katibu mkuu Mtendaji mpya wa Shirikisho hilo SAGOLE WAMBURA akiapa leo 
Viongozi wa TAHLISO wameapishwa leo rasmi Jijini Dar es salaam baada ya uchaguzi wa Kidemocrasia uliofanyika tarehe 23 mwezi huu na wataiongoza Taasisi hiyo kwa mwaka mmoja kwa mujibu wa katiba yao.
JOSEPH SHABAN ambaye ni muazini mpya wa shirikisho hilo Akiapa leo 
Omary Idd Naibu muazini akiapa leo tayari kulitumikia shirikisho hilo 
Mwenyikiti mpya wa shirikisho la wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania TAHLISO Ndugu STANSLAUS PETER akizungumza na wanahabari mara baada ya kuapishwa rasmi kuwatumikia wanafunzi wa elimu ya juu nchini 
Wanahabari waliokuwa katika hafla hiyo 


Picha za pamoja baada ya kula kiapo kwa viongozi hao wapya wa TAHLISO leo Jijini Dar es salaam 

No comments: