Serikali Haijatoa Tamko La Kutowalipa Makocha Wa Taifa Stars - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Friday, 25 December 2015

Serikali Haijatoa Tamko La Kutowalipa Makocha Wa Taifa Stars


Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inakanusha taarifa zilizoandikwa katika gazeti la Mwananchi la tarehe 24.12.2015 yenye kichwa cha habari “JPM kutolipa makocha Stars”.

Serikali  kupitia Wizara inayohusika na michezo haijatoa tamko  la kutowalipa makocha wanaofundisha timu ya Taifa Stars kama ilivyoripotiwa na gazeti hilo.

Suala la malipo ya makocha wa Taifa Stars linashughulikiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Serikali, pindi maamuzi yatapofikiwa, serikali itatoa maelekezo kama itaendelea kuwalipa au la.

Serikali ya Awamu ya Tano inathamini michezo yote ikiwemo mpira na miguu , kwa hiyo itaendelea kushirikiana na Vyama vya vyote vya michezo na wadau wote wa michezo kwa ujumla katika kuhakikisha kuwa michezo inaimarika na kuwa chanzo cha ajira kwa vijana nchini.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI (MAELEZO)

24 DESEMBA, 2015
Post a Comment