Rais Magufuli Afanya Mazungumzo Na Spika Wa Baraza La Seneti Na Mjumbe Maalum Wa Rais Wa Jamhuri Ya Burundi,pierre Nkurunzinza


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa  Seneti na Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Burundi Mheshimiwa Reverien Ndikuriyo Ikulu jijini Dar Es Salaam kuhusu  hali ya kisiasa na usalama nchini Burundi na jitihada zinazochukuliwa na Tanzania ikiwa ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Afrika Mashariki

Akiwasilisha ujumbe wa Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi kuhusu hali ya Burundi, Spika Ndikuriyo amesema Serikali ya Burundi ipo tayari kufanya mazungumzo na wadau wote wa siasa kuhusu hali ya Burundi na jitihada za kuumaliza mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini humo

Akitoa maelezo ya kikao hicho kwa niaba ya Rais Magufuli, Balozi Maiga amesema serikali ya Burundi imekubali usuluhishi unaofanywa na Rais wa Uganda Mh. Yoweri Kaguta Museveni kwa niaba ya Marais wa Jumuia ya Afrika Mashariki kutokana na kikao kilichofanyika Jijini Dar es salaam mwezi Julai mwaka huu na kwamba serikali ya Burundi iko tayari kushiriki katika mazungumzo hayo ya amani.

“Mheshimiwa Rais Magufuli amefanya mazungumzo na rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi mwishoni mwa wiki iliyopita ambaye amemuhakikishia Rais Magufuli utayari wake wa kushiriki katika mazungumzo hayo ya usuluhishi” Alisema Balozi Maiga .

Balozi Maiga ameongeza kuwa “nimeagizwa nilipeleke taarifa kwa mawaziri wa nchi za nje wa nchi jirani juu ya maandalizi ya mazungumzo hayo ambayo yataanza kule Uganda tarehe 28 mwezi Desemba na Waziri wa Ulinzi wa Uganda amekabidhiwa jukumu la kuratibu mazungumzo hayo”

Ameongeza kuwa suala jingine lililojitokeza katika mazungumzo hayo ni juu ya uamuzi wa baraza la usalama la umoja wa Afrika kutaka kupeleka majeshi yake nchini Burundi baada ya siku tano jambo ambalo Bunge la Burundi limepinga.

Balozi Mahiga amesema Burundi imepinga maamuzi hayo kwa kuwa inaamini kuwa hakuna hali ama dalili za kutokea kwa mauaji ya kimbari kama ya Rwanda, na kwamba kwa sasa kuna utulivu nchini humo tofauti na wasiwasi wa Umoja wa Afrika, Jumuia za kimataifa hasa Umoja wa Ulaya, na kwa kiwango fulani Umoja wa Mataifa unaotoa msukumo wa kutaka kuyapeleka majeshi ya kulinda amani nchini Burundi.

“Wao kama Burundi wakiwa ni washirika wakubwa wa kulinda amani katika bara la Afrika wana wanajeshi 6000 nchini Somalia,wanajeshi 1000 Jamhuri ya Afrika ya Kati na dhamira yao katika kushiriki kuleta amani, wao watakuwa ni watu wa mwisho kuleta hali itakayosababisha hatari ya kutokea kwa mauaji yanayofanana na mauaji ya kimbari” amesisitiza Balozi Mahiga

Dkt. Maiga amesema kutokana na maelezo hayo, Rais Magufuli amependekeza kuwa serikali ya Burundi ifungue milango ya mazungumzo na kuwakaribisha Umoja wa nchi za Kiafrika kupeleka ujumbe wa aina yeyote ili kwa pamoja waweze kutathmini hali usalama ilivyo nchini Burundi badala ya kukataa pendekezo hilo moja kwa moja.

Aidha, Balozi Mahiga amesema, Rais Magufuli amemuagiza kwenda nchini Burundi kutazama, kujiridhisha na kutathmini hali halisi ilivyo hususani katika suala la amani hasa ulinzi na usalama wa raia katika jiji la Bujumbura na maeneo mengine ya nchi hiyo ili kufahamu sababu zinazowafanya warundi kukimbia nchi yao na kukimbilia nchi majirani ikiwemo Tanzania kama wakimbizi.

Ameongeza kuwa safari yake ya kwenda Burundi kwa kiasi kikubwa itasaidia katika kuendeleza mazungumzo yanayotarajia kufanyika huko Uganda.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es Salaam.

22 Desemba, 2015
Previous
Next Post »
My photo

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
My goal with BLOG is to help you learn Electrical.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Label

KITAIFA NEWS KIMATAIFA MICHEZO BURUDANI SIASA TECHNICAL ARTICLES f HAPA KAZI TU. LEKULE TV EDITORIALS ARTICLES DC DIGITAL ROBOTICS SEMICONDUCTORS MAKALA GENERATOR GALLERY AC EXPERIMENTS MANUFACTURING-ENGINEERING MAGAZETI REFERENCE IOT FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY ELECTRONICS ELECTRICAL ENGINEER MEASUREMENT VIDEO ZANZIBAR YETU TRANSDUCER & SENSOR MITINDO ARDUINO RENEWABLE ENERGY AUTOMOBILE SYNCHRONOUS GENERATOR ELECTRICAL DISTRIBUTION CABLES DIGITAL ELECTRONICS AUTOMOTIVE PROTECTION SOLAR TEARDOWN DIODE AND CIRCUITS BASIC ELECTRICAL ELECTRONICS MOTOR SWITCHES CIRCUIT BREAKERS MICROCONTROLLER CIRCUITS THEORY PANEL BUILDING ELECTRONICS DEVICES MIRACLES SWITCHGEAR ANALOG MOBILE DEVICES CAMERA TECHNOLOGY GENERATION WEARABLES BATTERIES COMMUNICATION FREE CIRCUITS INDUSTRIAL AUTOMATION SPECIAL MACHINES ELECTRICAL SAFETY ENERGY EFFIDIENCY-BUILDING DRONE NUCLEAR ENERGY CONTROL SYSTEM FILTER`S SMATRPHONE BIOGAS POWER TANZIA BELT CONVEYOR MATERIAL HANDLING RELAY ELECTRICAL INSTRUMENTS PLC`S TRANSFORMER AC CIRCUITS CIRCUIT SCHEMATIC SYMBOLS DDISCRETE SEMICONDUCTOR CIRCUITS WIND POWER C.B DEVICES DC CIRCUITS DIODES AND RECTIFIERS FUSE SPECIAL TRANSFORMER THERMAL POWER PLANT cartoon CELL CHEMISTRY EARTHING SYSTEM ELECTRIC LAMP ENERGY SOURCE FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 2 BIPOLAR JUNCTION TRANSISTOR 555 TIMER CIRCUITS AUTOCAD C PROGRAMMING HYDRO POWER LOGIC GATES OPERATIONAL AMPLIFIER`S SOLID-STATE DEVICE THEORRY DEFECE & MILITARY FLUORESCENT LAMP HOME AUTOMATION INDUSTRIAL ROBOTICS ANDROID COMPUTER ELECTRICAL DRIVES GROUNDING SYSTEM BLUETOOTH CALCULUS REFERENCE DC METERING CIRCUITS DC NETWORK ANALYSIS ELECTRICAL SAFETY TIPS ELECTRICIAN SCHOOL ELECTRON TUBES FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 1 INDUCTION MACHINES INSULATIONS ALGEBRA REFERENCE HMI[Human Interface Machines] INDUCTION MOTOR KARNAUGH MAPPING USEUL EQUIATIONS AND CONVERSION FACTOR ANALOG INTEGRATED CIRCUITS BASIC CONCEPTS AND TEST EQUIPMENTS DIGITAL COMMUNICATION DIGITAL-ANALOG CONVERSION ELECTRICAL SOFTWARE GAS TURBINE ILLUMINATION OHM`S LAW POWER ELECTRONICS THYRISTOR USB AUDIO BOOLEAN ALGEBRA DIGITAL INTEGRATED CIRCUITS FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 3 PHYSICS OF CONDUCTORS AND INSULATORS SPECIAL MOTOR STEAM POWER PLANTS TESTING TRANSMISION LINE C-BISCUIT CAPACITORS COMBINATION LOGIC FUNCTION COMPLEX NUMBERS ELECTRICAL LAWS HMI[HUMANI INTERFACE MACHINES INVERTER LADDER DIAGRAM MULTIVIBRATORS RC AND L/R TIME CONSTANTS SCADA SERIES AND PARALLEL CIRCUITS USING THE SPICE CIRCUIT SIMULATION PROGRAM AMPLIFIERS AND ACTIVE DEVICES BASIC CONCEPTS OF ELECTRICITY CONDUCTOR AND INSULATORS TABLES CONDUITS FITTING AND SUPPORTS CONTROL MOTION ELECTRICAL INSTRUMENTATION SIGNALS ELECTRICAL TOOLS INDUCTORS LiDAR MAGNETISM AND ELECTROMAGNETISM PLYPHASE AC CIRCUITS RECLOSER SAFE LIVING WITH GAS AND LPG SAFETY CLOTHING STEPPER MOTOR SYNCHRONOUS MOTOR AC METRING CIRCUITS APPS & SOFTWARE BASIC AC THEORY BECOME AN ELECTRICIAN BINARY ARITHMETIC BUSHING DIGITAL STORAGE MEMROY ELECTRICIAN JOBS HEAT ENGINES HOME THEATER INPECTIONS LIGHT SABER MOSFET NUMERATION SYSTEM POWER FACTORS REACTANCE AND IMPEDANCE INDUCTIVE RESONANCE SCIENTIFIC NOTATION AND METRIC PREFIXES SULFURIC ACID TROUBLESHOOTING TROUBLESHOOTING-THEORY & PRACTICE 12C BUS APPLE BATTERIES AND POWER SYSTEMS ELECTROMECHANICAL RELAYS ENERGY EFFICIENCY-LIGHT INDUSTRIAL SAFETY EQUIPMENTS MEGGER MXED-FREQUENCY AC SIGNALS PRINCIPLE OF DIGITAL COMPUTING QUESTIONS REACTANCE AND IMPEDANCE-CAPATIVE RECTIFIER AND CONVERTERS SEQUENTIAL CIRCUITS SERRIES-PARALLEL COMBINATION CIRCUITS SHIFT REGISTERS BUILDING SERVICES COMPRESSOR CRANES DC MOTOR DRIVES DIVIDER CIRCUIT AND KIRCHHOFF`S LAW ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS 1 ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS B ELECTRICAL TOOL KIT ELECTRICIAN JOB DESCRIPTION LAPTOP THERMOCOUPLE TRIGONOMENTRY REFERENCE UART WIRELESS BIOMASS CONTACTOR ELECTRIC ILLUMINATION ELECTRICAL SAFETY TRAINING FILTER DESIGN HARDWARE INDUSTRIAL DRIVES JUNCTION FIELD-EFFECT TRANSISTORS NASA NUCLEAR POWER SCIENCE VALVE WWE oscilloscope 3D TECHNOLOGIES COLOR CODES ELECTRIC TRACTION FEATURED FLEXIBLE ELECTRONICS FLUKE GEARMOTORS INTRODUCTION LASSER MATERIAL PID PUMP SEAL ELECTRICIAN CAREER ELECTRICITY SUPPLY AND DISTRIBUTION MUSIC NEUTRAL PERIODIC TABLES OF THE ELEMENTS POLYPHASE AC CIRCUITS PROJECTS REATORS SATELLITE STAR DELTA VIBRATION WATERPROOF