Madereva Watakaozidisha Abiria Kwenye Vyombo Vya Usafiri Kukiona - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Thursday, 24 December 2015

Madereva Watakaozidisha Abiria Kwenye Vyombo Vya Usafiri Kukiona


JESHI la Polisi Nchini limewatahadharisha madereva  watakaozidisha  idadi ya abiria kuliko uwezo wa chombo cha usafari kwani ni kosa kisheria na watakaozidisha abiria kwenye vyombo vyao vya usafiri watachukuliwa hatua za kisheria.

Operesheni hiyo inaanza leo baada ya tamko la Jeshi la Polisi na kuanza kutekeleza kwa wale wote wataobeba abiria wengi tofauti na uwezo wa basi. Watakaochukuliwa hatua ni madereva wa daladala,mabasi ya mikoani pamoja na magari aina ya Noah.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba amesema kuwa Jeshi la polisi linaanza operesheni ambayo ni endelevu na kuwataka watu wafuate sharia ya ubebaji wa abiria.

Advera amesema kuwa katika kipindi hiki cha siku kuu Jeshi la polisi limejipanga katika kuwadhibiti waendesha bodaboda kwa wataopandisha watu zaidi  ya wawili (mishikaki) kukiona cha mtema kuni kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani.


Aidha amewataka wananchi kutoa taarifa za kihalifu katika msimu wa sikukuu ili  kuimarisha  ulinzi wa watu na mali zao ili maisha yaweze kuendelea baada ya sikukuu.
Post a Comment