Ligi Kuu ya Zanzibar: JKU yaitandika KVZ bao 2-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Amaan - LEKULE

Breaking

31 Dec 2015

Ligi Kuu ya Zanzibar: JKU yaitandika KVZ bao 2-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Amaan

Wachezaji wa Timu ya JKU wakisalimiana na Wachezaji wa Timu ya KVZ kabla ya kuaza mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya JKU imeshinda 2-0.

Mchezo uliochezwa jioni mabao ya JKU yamefungwa katika kipindi cha kwanza na katika dakika ya 8 mshambuliaji wa Timu ya JKU Mbarouk Chande ameipatia bao timu yake katika dakika ya nane ya mchezo huo kipindi cha kwanza na Bao la ushindi la JKU limepatikana katika kipindi hicho cha kwanza katika dakika ya 35 ya mchezo huo lililofungwa na mshambuliaji wake Nassor  Mattar.
Kocha Mkuu wa Timu ya KVZ King akifuatilia mchezo huo wakati timu yake ikiwa nyuma kwa mabao 2-0. 
Beki wa timu ya KVZ Juma Abdalla, akijiandaa kumzuiya mshambuliaji wa Timu ya JKU mwenye mpira Nassorv Mattar, wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar. 
Mshambuliaji wa Timu ya JKU Mbarouk Chande(kulia) akimpita beki wa Timu ya KVZ Emill Wiliam  


Mshambuliaji wa Timu ya JKU Mbarouk Chande, akimiliki mpira huku beki wa timu ya KVZ Emill William akijiandaa kumzuiya.  
Mshambuliaji wa Timu ya JKU Mohammed Abdalla akimpiga chenga golikipa wa timu ya KVZ Yakub Bakari. hatimai mpira huo na kutoka nje ya uwanja. 


Mshambuliaji wa Timu ya KVZ Masoud Abdalla mwenye jezi ya kijani akimpita mchezaji wa timu ya JKU  Mbarouk Chande. 

No comments: