Jopo
la Watu Mashuhuri la Umoja wa Mataifa la Kupendekeza Namna Bora ya
Dunia Kukabiliana na Majanga ya Afya limekamilisha kazi yake wiki
iliyopita jijini New York.
Jopo
hilo linaloongozwa na Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete lilikabidhiwa
jukumu hilo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki moon tarehe 2
Aprili, 2015 na kupewa muda wa kuanzia Mei hadi Desemba 2015 kukamilisha
kazi yake.
Jopo
limefanya mikutano minne na kukutana na wadau mbalimbali wa afya
zikiwemo taasisi za Umoja wa Mataifa, wadau wa maendeleo, wataalam
mbalimbali na kupokea maoni na uzoefu kutoka kwa nchi zilizoathirika na
ugonjwa wa Ebola.
Watu
mashuhuri wanaounda Jopo hilo ni Mheshimiwa Michelin Calm-Roy aliyekuwa
Rais wa Shirikisho la Uswisi; Mheshimiwa Marty Natelagawa aliyekuwa
Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia; Mheshimiwa Joy Phumaphi, aliyekuwa
Waziri wa Afya wa Botswana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Mheshimiwa
Celso Amorim aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil na Rajiv Shah
aliyekuwa Mkuu wa Shirika la Misaada na Maendeleo la Marekani (USAID).
Jopo
hilo linatarajia kuwasilisha ripoti yake kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa mwezi January, 2016 na baadae kuwasilishwa kwenye Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Mwenyekiti wa Jopo, Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akiendesha Mkutano wa Jopo.
Wajumbe wa Jopo katika Picha ya Pamoja na Wajumbe wa Sekretariati ya Jopo.
Wajumbe wa Jopo la Watu Mashuhuri la Umoja wa Mataifa la Kushauri Dunia Namna Bora ya Kukabiliana na Majanga
No comments:
Post a Comment