Ben Pol kamwomba radhi Alikiba. - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Thursday, 24 December 2015

Ben Pol kamwomba radhi Alikiba.Jana December 23 2015 gossic cop wa show ya XXL #CloudsFM, Soudy Brown alifanikiwa kumpata Alikiba… maswali ya Soudy kwa Alikiba ilikuwa jinsi alivyopokea maneno ya Ben Pol kwenye post ya Twitter ambayo alimtaja !!
Alikiba alisema hana neno na wala hana tatizo na Ben Pol, kwa hiyo hata kilichoandikwa na Ben Pol alikichukulia poa kabisa… leo Alikiba alikuwa ‘live’ kwenye show ya Jahazi Clouds FM, baada ya stori mbili tatu watangazaji Emmanuel Likuda na ‘Mtembezi’ Antonio Nugaz wakaona wamcheki pia Ben Pol ili kujua sababu ya kuweka post ya kumhusu Alikiba na muziki wake.
ALIKIBA II
Mtangazaji Emmanuel Likuda na Alikiba
Unajua Alikiba ni kama kaka, alivyolichukulia hili suala najua kalichukulia kama kaka… suala la msingi, Watanzania wajue kwamba tuko sawa na Kiba… tukiwa tunazunguka haitakuwa kitu kizuri… tutakiane heri kwa sababu tumekuwa na mwaka mzuri.’- Ben Pol.


Kwenye sentensi nyingine Ben Pol ameendelea hivi >>> ‘Haijalishi nani kajishusha kuomba radhi lakini suala la msingi ni kwamba mimi na Kiba tuko sawa…
Ben-Pol
Ben Pol


Alikiba nae akaongea haya wakati Ben Pol akiwa hewani bado >>> ‘Nimekusamehe lakini nilishtushwa kama watu wengine walivyoshtuka… ni binadamu tunakuwa na makosa wakati mwingine…


Ben Pol nae akamalizia >>> ‘Huwezi jua mipango ya MUNGU, hatujui hapo mbeleni inaweza kutokea bonge la collabo yetu


Sehemu ya interview hiyo nimeirekodi na kukuwekea hapa, unaweza kuplay kuisikiliza yote kama ulipiitwa kwenye Jahazi.


Post a Comment