Askofu Morogoro Amtaka Rais Magufuli Kuendeleza 'moto' ili Kuwadhibiti Wapiga Dili - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Friday, 25 December 2015

Askofu Morogoro Amtaka Rais Magufuli Kuendeleza 'moto' ili Kuwadhibiti Wapiga Dili

Serikali ya awamu ya tano imeshauriwa kuendelea na adhma yake ya kudhibiti watumishi wa umma wanaotumia madaraka yao vibaya kwa maslahi binafsi.

Katika kuadhimisha sikukuu ya Krisimas mkoani Morogoro Askofu mkuu wa kanisa la KKKT Dayosisi ya Morogoro Askofu Jackob Mameo ameiomba serikali kuendelea na msimamo wake wa kuwawajibisha watumishi wanaotumia nafasi zao kwa manufaa binafsi ili wananchi hasa wanaoishi vijijini wanufaike na rasilimali za taifa lao.

Akiongoza ibada ya misa ya sikukuu ya Krismas Askofu Mameo amepongeza juhudi za serikali ya awamu ya tano ambapo amesema asilimia kubwa ya wananchi wa vijijini wanaishi katika mazingira magumu kwa kukosa huduma muhimu za maji, umeme pamoja na miundombinu bora ya barabara…

kwa upande wao waumini wa kikristo wameomba vyombo vya ulinzi kuhakikisha wanalinda usalama katika maeneo yote yenye mkusanyiko wa watu ili kuepusha uvunjifu wa amani unaoweza kujitokeza ambapo pia wamewataka watanzania kusherekea sikukuu hii ya krismas kwa amani na utulivu bila kubaguana


Post a Comment