Ofisa Uhusiano wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Joseph Ngowi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam , kuhusu maadhimisho ya Siku ya Posta duniani, inayoadhimishwa, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) jijini, kabla ya kumkaribisha Meneja Masoko wa shirika hilo, David George (kulia) kuzungumza masuala mbalimbali yanayohusu maadhimisho ya siku hiyo, leo jijini Dar.
Meneja Masoko wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), David George, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu maadhimisho ya Siku ya Posta duniani, inayoadhimishwa kesho, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) jijini. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano, Elia Madulesi.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakichukua habari na kumsikiliza Meneja Masoko wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), David George, wakati akizungumza nao, jijini Dar es Salaam jana, kuhusu maadhimisho ya Siku ya Posta duniani, inayoadhimishwa kesho, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) jijini. Kulia ni Ofisa Uhusiano Mwandamizi Mkuu wa TPC, Wilfred Miigo.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza Meneja Masoko wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), David George, wakati akizungumza nao, jijini Dar es Salaam jana, kuhusu maadhimisho ya Siku ya Posta duniani.
Meneja Masoko wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), David George, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati alipokuwa akizungumza nao jijini, Dar es Salaam jana, kuhusu maadhimisho ya Siku ya Posta duniani, inayoadhimishwa leo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) jijini.
Na Mwandishi Wetu
UKUAJI wa Sayansi na Teknolojia ya habari hapa nchini kama mitandao ya simu za mkononi imeathiri kwa kiasi kikubwa huduma za uandishi wa barua na kutuma kwa njia ya posta.
Hayo, yameelezwa Dar es Salaam jana na Meneja Masoko wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), David George kwa niaba ya Kaimu  Postamasta Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo, Fortunatus Kapinga, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jkuhusu Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani.
Maadhimisho hayo, yanayofanyika leo duniani kote nchini Tanzania yatafanyika Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), ambapo alisema kutokana na ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano uandikaji wa barua umekuwa ukiathiriwa kwa kiasi kikubwa kwani watu wengi wamekuwa wakiwasiliana kwa njia ya simu kupitia meseji fupi (SMS).
“Kutokana na athari hizo, shirika limeamua kuanzisha shindano la uandishi wa Insha kwa wananfunzi wa Shule za Msingi na Sekondari ambapo washindi 10 wa shindano hilo watapata zawadi mbali mbali, ikiwemo vifaa vya shule vya kusomea na kujifunzia,”alisema.
Alisema shindano hilo, limekuwa likiwaongezea wanafunzi hao hamasa ya uandishi wa barua kwani vijana wengi wa sasa hawajui hata kuandika barua za kikazi kwani hata maombi ya kazi huangalia kwenye mtandao au kutuma taarifa kwa njia ya mtandao.
“Katika uandishi wa isha hizo tuliweka mada ya tueleze juu ya dunia unayopenda kukulia, yenye kauli mbiu  ya ubunifu, utangamano na ushirikishwaji ni vichocheo muhimu kwa mustakabali wa posta,”alisema.
Ofisa huyo, alisema kutokana na ubunifu na utengamano na ushirikishwaji imekuwa ni kichocheo katika kufanikisha malengo ya shirika hilo, ikiwa ni pamoja na matumizi ya  teknolojia  ya habari na mawasiliano (Tehama).
“Tunaendelea kutekeleza mfumo wa Tehama ujulikanao kama ‘Postal Global’ ambao hadi sasa ofisi 95 zimeunganishwa ambapo lengo letu ni kuunganisha ‘on line’ ofisi zote ili kuwe na huduma jumuishi za kimtandao,”alisema.
Katika maadhimisho hayo, washindi watatu wa insha watatunukiwa zawadi zao.
Pia Shirika katika kuadhimisha siku hiyo, alisema kuwa wamekusudia leo kwenda kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi katika Taasisi ya saratani ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.