Muandishi Wa habari Amfukuzisha Kazi Kocha Wa Mexico - LEKULE

Breaking

29 Jul 2015

Muandishi Wa habari Amfukuzisha Kazi Kocha Wa Mexico

Shirikisho la soka nchini Mexico (FMF), limemfuta kazi kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo Miguel Herrera, baada ya kujiridhisha alionyesha utovu wa nidhamu wakati wa kufurahia ubingwa wa ukanda wa Amerika ya kati, kaskazini na visiwa vya Caribbean (CONCAFAC Gold Cup) mwishoni mwa juma lililopita.
 Raisi wa shirikisho la soka nchini Mexico akiongeza na waandidhi wa habari.

Raisi wa shirikisho la soka nchini humo Decio de Maria, alithibitisha kumfuta kazi kocha huyo kwa kusema Herrera amebainika alimsukuma muandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Mexico (TV Azteca), Christian Martinoli ambaye kila wakati alikiponda kikosi cha mabingwa hao wa CONCACAF.

Decio de Maria, amesema wamechukua maamuzi hayo baada ya kufanya uchunguzi ikiwa ni pamoja na kumuhoji Herrera na Christian Martinoli ambapo kila mmoja alieleza uhalisia wa tukio lilivyokua.
mwandishi anayedai kusukumwa na kocha wa mexico
Tukio la kusukumwa kwa Christian Martinoli lilitokea kwenye uwanja wa ndege Philadelphia wakati wa safari ya kikosi cha Mexico kilipokua kikirejea nyumbani.
Hata hivyo rais wa shirikisho la soka nchini Mexico, De Maria amesema kocha Herrera baada ya kufanya hivyo aliomba radhi kupitia katika kituo kimoja cha radio cha nchini Mexico, lakini haikutosha kuwashawishi kukubali msamaha huo

alisukumwa na Herrera, alianza kukikandia kikosi cha timu ya taifa ya Mexico, baada ya kushindwa kufanya vyema kwenye michuano ya Ukanda wa Amerika ya kusini (Copa Amerika) iliyofanyika nchini Chile, hususan walipotolewa katika hatua ya makundi.
Kufuatia maamuzi ya kutimuliwa kwa Miguel Herrera, kunaufanya uongozi wa shirikisho la soka nchini Mexico kuanza mchakato wa kumsaka mrithi wake, na tayari rais De Maria amesisitiza kuhitimisha zoezi hilo itakapofika mwezi Septemba.
Mexico walitawazwa kuwa mabingwa wa CONCACAF Gold Cup mwaka 2015 baada ya kuibanjua timu ya taifa ya Jamaica mabao matatu kwa sifuri katika mchezo wa hatua ya fainali uliounguruma mjini Philadelphia nchini Marekani mwishoni mwa juma lililopita.

No comments: