Aunt azua minong’ono ukumbini usiku - LEKULE

Breaking

30 Jul 2015

Aunt azua minong’ono ukumbini usiku


STAA wa kiwango cha juu kupitia filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson, kwa mara ya kwanza tangu ajifungue, amezua minong’ono ukumbini.
Mpango mzima ulishuhudiwa usiku kwenye Ukumbi wa Ngome Kongwe, Zanzibar ambapo kulikuwa na Tamasha la Kimataifa la Filamu (ZIFF) ambapo Aunt alitinga akiwa na baadhi ya mastaa wenzake huku baadhi ya watu wakishangaa na kunong’ona kuwa mtoto wake bado ni mdogo iweje awe ukumbini  badala ya kuwa naye muda huo.
“Mmmmh huyu siyo Aunt kweli? Jamani mtoto wake mbona bado mdogo sana kwa nini amekuja ukumbini usiku wote huu?” alihoji mmoja wa watu waliokuwa ukumbini humo.

mtandao huu ulipozungumza na Aunt kuhusiana na minong’ono hiyo alisema: “Niko makini san-a kwa upande wa mtoto, hapa nilipo nikitoka nje tu naona hoteli niliyofikia na mwanangu hivyo hakuna shida na siwezi kuja na mtoto hapa kwenye mkusanyiko wa watu wengi,” alisema Aunt.


No comments: